Nchimbi: Nitafikisha agenda ya kikokotoo kwa Rais Samia

By Halfani Chusi , Nipashe
Published at 06:26 PM Apr 15 2024
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, (CCM) Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi.
Picha: Halfani Chusi
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, (CCM) Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi.

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, (CCM) Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi ameahidi kuifikisha hoja ya kikokotoo kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwaajili ya utatuzi akisistiza imekuwa kero kubwa kwa wastaafu.

Pia amewataka waliopewa zabuni ya kujenga Uwanja wa Ndege wa mkoani Rukwa kuongeza kasi ili kuendana na  matakwa ya mkataba.

Nchimbi ameyasema hayo leo mkoani Rukwa, alipokagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo na kisha baadaye kufanya mkutano wa hadhara na wananchi ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea mikoa sita.

"Tatizo la kikokotoo linalalamikkwa sana na watumishi, imekuwa kero kubwa Kuna muda lazima tuangalie wananchi wetu, wanachama wetu, tuangalie tutafika wapi lakini kwa kadri inavyowezekana tunapaswa kutatua kero za wananchi," amesema na kuongeza kuwa;

"Nitalifikisha suala hilo Katika uongozi wa juu kuona namna ya kulitafutia ufumbuzi kwakuwa lengo la CCM ni kutatua kero za wananchi" amesema Nchimbi