TEHAMA iwe kichocheo kwenye tathmini na ufuatiliaji wa takwimu

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 08:31 PM Apr 15 2024
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dk. John Jingu.
Picha: Mpigapicha Wetu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dk. John Jingu.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dk. John Jingu amesema Matumizi na Teknolojia ya habari iwe ni kichocheo cha kufanya ufuatiliaji na tathmini ili kupata takwimu sahihi zitakazo changia kufanya maamuzi sahihi wakati wa kuandaa mipango ya bajeti kwenye Sekta ya Afya.

Dk. Jingu amesema hayo wakati akifungua kikao cha siku mbili, Aprili 15, 2024 jiji Arusha, kilichowakutanisha wataalam wa Tehama na wale wa ufuatiliaji na tathmini zaidi ya 70 kwa lengo la kukuza ushirikiano baina ya wadau hao, uboreshaji wa program na maendeleo ya jumla ya utoaji wa huduma kwenye kwenye sekta ya afya ili kuwa na takwimu sahihi. 

Dk. Jingu amesema ukuaji wa Teknolojia uende sambamba na mabadiliko ya mifumo ya TEHAMA kwa kuiunganisha ili iweze kusomana hali itakayochangia kuwa na tija na ufanisi wakati wa utekelezaji wa majukumu kwenye sekta afya na kupata matokeo chanya.