Burhani ataka uvumilivu sera mpya ya mikopo kwa vijana

By Vitus Audax , Nipashe
Published at 10:28 AM Apr 15 2024
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kagera Faris Burhani.

MWENYEKITI wa UVCCM Mkoa wa Kagera Faris Burhani amewataka vijana mkoani humo hususani maofisa usafirishaji maarufu kama bodaboda kuendelea kuwa wavumilivu wakati serikali inaendelea na maboresho ya sera ya mikopo ya vijana, wanawake na watu mwenye ulemavu.

Mikopo hiyo ilisitishwa na  serikali kutokana  na baadhi ya vikundi kukopa fedha bila kurejesha kwa Wakati sambamba na udanganyifu katika utolewaji wa mikopo hiyo.

Burhani ametoa rai hiyo wakati  akiongea na wananchi  pamoja na bodaboda wa Kata ya Kabindi  Wilaya ya Biharamulo  mkoani Kagera katika ziara yake ya  kikazi ya siku 16 iliyoanza Aprili 14 katika Wilaya hiyo.