Kenya Airways yasitisha safari zake kuelekea Kinshasa

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 03:33 PM Apr 30 2024
Ndege ya Kenya Airways.
PICHA: MAKTABA
Ndege ya Kenya Airways.

SHIRIKA la ndege la Kenya, Kenya Airways limesema litasitisha safari za ndege kuelekea Mji Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Kinshasa, baada ya mamlaka ya kijeshi kushindwa kuwaachilia wafanyakazi wake iliowazuia licha ya amri ya mahakama.

Idara ya ujasusi ya jeshi la Congo iliwashikilia wafanyakazi wawili wa Kenya Airways tarehe 19 Aprili kwa madai ya kushindwa kujaza nyaraka za forodha kwenye baadhi ya mizigo ya thamani, na shirika hilo la ndege linasema idara hiyo imepinga kuwaachilia wafanyakazi hao licha ya amri ya mahakama ya kijeshi.

“Kutokana na kuendelea kuzuiliwa kwa wafanyakazi wa KQ na kitengo cha idara ya ujasusi ya jeshi mjini Kinshasa, shirika hilo la ndege haliwezi kuendelea na safari zake kwa ufanisi bila wafanyakazi hao, shirika hilo limesema katika taarifa.

“Kama matokeo, tumefikia uamuzi mgumu wa kusitisha safari kuelekea Kinshasa kuanzia tarehe 30 Aprili hadi tutakapoweza kufanya safari hizi kwa ufanisi.”