Wizara ya Madini imewasilisha hoja ya Bajeti Bungeni leo

By Frank Monyo , Nipashe
Published at 10:46 PM Apr 30 2024
news
Picha: Wizara Madini.
Waziri wa Madini, Anthony Mavunde

Waziri wa Madini, Antony Mavunde Leo anawasilisha Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Madini kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025.

"Kwa namna ya kipekee nitumie  fursa hii adhimu kutoa shukrani zangu za dhati kwa  Mheshimiwa Rais kwa kuniamini na kunipa dhamana ya  kusimamia Sekta ya Madini. Ni ahadi yangu kwa  Mheshimiwa Rais, na Bunge lako Tukufu pamoja na  Watanzania kwamba nitaitumikia nafasi hii kwa  uadilifu, uaminifu na kwa uwezo wangu wote ili  kuendeleza sekta hii muhimu"- Mhe. Antony Mavunde, Waziri wa Madini