Adel Amrouche kwenda CAS kukata rufaa

By Dotto Charles , Nipashe
Published at 12:27 PM Apr 16 2024
kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Adel Amrouche.
PICHA: MAKTABA
kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Adel Amrouche.

KOCHA wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Adel Amrouche, anatarajia kwenda kukata rufaa katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo ya FIFA maarufu CAS baada ya kufungiwa mechi nane na Shirikisho la Soka Afrika kutokana na matamshi yake yaliyozua utata katika mashindano ya Kombe la Afrika AFCON.

Hivi karibuni kilifanyika kikao katika kujadili suala la kocha huyo ambapo halikupatiwa mwafaka licha ya kufutiwa faini ya Euro 9200.

Adel Amrouche alifungiwa na Kamati ya Nidhamu ya CAF, malalamiko yaliyowasilishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Morocco (RMFF) dhidi ya Kocha Amrouche likimlalamikia Kocha huyo kwa kauli zake kuwa Morocco inaushawishi ndani ya CAF katika kupanga mechi pamoja na waamuzi.

Kufuatia adhabu hiyo, Kamati ya Utendaji ya TFF pia ilimsimamisha kocha huyo na kumteua Hemed Morocco kuwa Kaimu Kocha akiisaidiana na Juma Mgunda.