Mo Dewji afanya kikao kizito na viongozi wa Simba

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 01:05 PM Apr 15 2024
Rais wa Heshima Klabu ya Simba SC Mohammed Dewji akiongoza kikao na viongozi wa Simba.
Picha: Mo Dewji
Rais wa Heshima Klabu ya Simba SC Mohammed Dewji akiongoza kikao na viongozi wa Simba.

Rais wa Heshima Klabu ya Simba SC Mohammed Dewji amefanya kikao na viongozi kujua changamoto zinazoikabili na kuzitatua timu hiyo kwa sasa.

Kupitia mitandao yake ya kijamii Mo Dewji ameandika:

“Nimefanya kikao na viongozi wa Simba SC kujua changamoto zipo wapi na namna ya kuzitatua. Kikao kimeenda vizuri. WanaSimba tusife moyo, tuendele kushirikiana.”

Baadhi ya Viongozi walioshiriki kikao hicho ni pamoja na Mwenyekiti wa Bodi Simba Salim Abdallah Muhene (Try Again), Mwenyekiti wa zamani Simba Swedi Nkwabi na Mshauri wa Mo Dewji, Crescentuis Magori.